VIJANA ZAIDI YA 70 WANUFAIKA NA MRADI WA KUIJIONGEZEA KIPATO

VIJANA ZAIDI YA 70 WANUFAIKA NA MRADI WA KUIJIONGEZEA KIPATO

Like
311
0
Friday, 30 January 2015
Local News

VIKUNDI saba vya vijana na wanawake vyenye wanachama 73 wamenufaika kwa kupata mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 7 kwa ajili ya kuanzisha biashara na kujikwamua kiuchumi.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa, DoktaLeticia Warioba wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema vijana zaidi ya 70 wamepatiwa vifaa na mbegu na wamelima zaidi ya ekari 70 katika kijiji cha Isimani ikiwa ni mradi wa kujiongezea kipato.

Amesema vijana hao wamepatiwa mikopo hiyo kwa ajili ya kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kuweza kujikwamua na umaskini na kuboresha maisha yao.

Comments are closed.