VIKAO VYA KAMATI YA BUNGE VIMEENDELEA LEO JIJINI DAR

VIKAO VYA KAMATI YA BUNGE VIMEENDELEA LEO JIJINI DAR

Like
454
0
Tuesday, 21 October 2014
Local News

VIKAO vya kamati za Bunge vimeendelea leo jijini Dar es salaam ikiwa ni siku ya pili ambapo ripoti za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma zimewasilishwa zikifatiwa na taarifa ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2012-2013 Katika Kamati ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma-PAC.

Akisoma Ripoti ya CAG, mbele ya mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe, Msaidizi Mkaguzi Mkuu Nestory Karia amesema ofisi yake imebaini mapungufu mengi ya fedha katika baadhi ya mashirika ikiwemo Chuo cha Veta, Bodi ya Mikopo na Shirika la Umeme Tanesco.

Comments are closed.