VIKWAZO ZAIDI DHIDI YA URUSI KUJADILIWA BRUSSELS

VIKWAZO ZAIDI DHIDI YA URUSI KUJADILIWA BRUSSELS

Like
252
0
Thursday, 29 January 2015
Global News

MAWAZIRI wa mambo ya nje kutoka Ulaya watakutana mjini Brussels kujadili vikwazo zaidi dhidi ya Urusi kufuatia mashambulizi ya Mashariki mwa Ukraine.

Mkutano huu wa dharula umeitishwa baada ya raia 30 kuuawa kwa makombora, mauaji yaliyotekelezwa na Waasi wanaodaiwa waliungwa mkono na Urusi na kushambulia bandari ya Mariupol Mwishoni mwa wiki iliyopita.

Majeshi ya NATO yamesema mamia ya vifaru vya Urusi, Magari ya Silaha yalikua Mashariki mwa Ukraine, ingawa Urusi imekana kujihusisha moja kwa moja na mashambulizi hayo.

 

 

Comments are closed.