VIONGOZI watatu wa kanisa la Baptist nchini Guinea wamepigwa na kisha kutekwa nyara baada ya wenyeji kudhani kwamba walikuwa maafisa wanaohamasisha jamii dhidi ya ugonjwa wa Ebola .
Viongozi hao walikuwa wametembelea kijiji cha kabac eneo la forecariah wakilenga kufukiza dawa ya wadudu kwenye kuta za vyoo vya umma ikiwa ni sehemu pia ya kujipatia huduma ya maji .
Taarifa zimesema kuwa wanakijiji hao walipowaona waliwashuku kuwa wanataka kueneza ugonjwa wa ebola katika eneo hilo .