VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI WAMETAJWA KUWA CHANZO CHA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI

VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI WAMETAJWA KUWA CHANZO CHA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI

Like
228
0
Friday, 05 June 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa migogoro ya Ardhi hapa Nchini inasababishwa na baadhi ya Viongozi wa Serikali za Mitaa  na Vijiji wasiokuwa na uelewa mpana kuhusu maswala ya sheria na utaratibu wa ugawaji ardhi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mwemwekiti wa Jukwaa la Ardhi Tanzania Docta STEPHEN MUNGA amesema kuwa suala la migogoro ya ardhi limekuwa ni changamoto kubwa katika jamii hususani ya wakulima na wafugaji ambao wamekuwa na madai ya mara kwa mara katika maeneo yao.

MUNGA ameongeza kuwa ili kuondokana na changamoto hiyo inapaswa kuwepo kwa utaratibu mzuri wa utoaji ardhi  kwa kuzingatia sera ya utawala bora na maadili ya uongozi.

Comments are closed.