VITUO VYA KUANDIKISHA WAPIGA KURA VYAANDALIWA MTWARA

VITUO VYA KUANDIKISHA WAPIGA KURA VYAANDALIWA MTWARA

Like
459
0
Tuesday, 18 November 2014
Local News

 

VITUO 111 vya kuandikisha wapiga kura na kupigia kura vimeandaliwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani humo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo LIMBAKISYE SHIMWELA wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake kuhusu idadi ya Vituo hivyo ambavyo tayari vimeandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Amebainisha kuwa Serikali imejiandaa kufanya Uchaguzi huo ifikapo Desemba 14 mwaka huu na kwamba anaamini utafanyika kwa mafanikio makubwa ili taifa lipate viongozi Bora.

 

Comments are closed.