WAASI Nchini Sudani kusini wamewaachia huru kundi la kwanza la watoto waliokuwa wamechukuliwa kuwa wanajeshi, kundi hilo la watoto lililotegemewa kuachiwa wiki chache zijazo.
Shirika la kimataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limesema Watoto mia mbili na themanini, wengine wakiwa wadogo wa mpaka umri wa miaka 11 walikabidhiwa katika jimbo la jonglei kwa ajili ya kukutanishwa na Familia zao.
Kundi la walioachiwa ni sehemu ya Jeshi la waasi linaloongozwa na David Yau Yau ambaye alisaini mkataba wa amani na Serikali mwaka mmoja uliopita.