WABUNGE WAWATAKA VIONGOZI KUFANYA TATHIMINI YAKUTOSHA JUU YA MASWALI MBALIMBALI YANAYOULIZWA

WABUNGE WAWATAKA VIONGOZI KUFANYA TATHIMINI YAKUTOSHA JUU YA MASWALI MBALIMBALI YANAYOULIZWA

Like
248
0
Wednesday, 04 February 2015
Local News

 WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, wamewataka viongozi wa serikali hususani mawaziri na manaibu wao kufanya tathimini ya kutosha juu ya maswali mbalimbali yanayoulizwa ili kutoa majibu sahihi naya kuridhisha kwa manufaa ya Taifa.

Wito huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na mbunge wa kigoma kaskazini mheshimiwa ZITTO KABWE wakati akiomba mwongozo kufuatia majibu yaliyotolewa na Naibu waziri wa Nishati na Madini mheshimiwa CHARLES MWIJAGE kwa baadhi ya maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwa wizara hiyo katika kipindi cha maswali na majibu.

Mheshimiwa ZITTO amesema kuwa ni vyema kwa masuala yote muhimu kutolewa ufafanuzi wa kutosha ili kusaidia kuleta uelewa kwa wahusika hali iliyosababisha mwenyekiti wa kikao cha leo mheshimiwa MUSSA AZAN kumsihi naibu waziri kurudia kutoa majibu katika muda wao binafsi.

Comments are closed.