Wachina 3 kufikishwa mahakamani Nairobi kufuatia sakata ya tikiti treni SGR

Wachina 3 kufikishwa mahakamani Nairobi kufuatia sakata ya tikiti treni SGR

Like
625
0
Monday, 26 November 2018
Global News

Raia watatu wa China wanaofanya kazi na reli mpya nchini Kenya SRG watafikishwa mahakamani baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika kwenye sakati ya tikiti.

Hii ni baada ya mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya kuidhinisha tume ya kupambana na ufisadi kuwafungulia mashtaka raia hao watatu wa China.

Li Gen, anayesimamia usafiri , Li Xiaou meneja wa ulinzi na Sun Xin ambaye ni mfanyakazi watafunguliwa mashtaka ya kujaribu kuwahonga maafisa waliokuwa wanachunguza sakata hiyo ya tikiti.

Watatu hao wanaripotiwa kujaribu kuwahonga maafisa wa uchunguzi shilingi 500,000 za Kenya au dola 5,000. Walikamatwa Ijumaa na maaafisa kutoka tume ya kupambana na ufisadi EACC.

Polisi wanasema wafanyabiashara wengine wamechukua wajibu wa kuwaletea wasafiri tikiti ambao hawataki kusumbuka kwa kupanga foleni ndefu.

Ukizungumzia suala hilo ubalozi wa China mjini Nairobi kupitia mkurugenzi wake wa mawasiliano Zhang Gang alisema Ubalozi unaheshimu uchunguzi unaofanywa na mamlaka za Kenya kuambatana na sheria za Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *