WAFANYABIASHARA wadogo wadogo katika soko la kariakoo wameiomba serikali kuweka wazi kuhusu posho wanazotozwa kila siku na polisi jamii.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na EFM katika soko la kariakoo leo jijini Dar es Salaam wamesema wamekuwa wakitozwa shilingi elfu 2 kwa kila askari anaepita katika biashara zao bila kujua matumizi ya fedha wanazotozwa.
Naye mmoja wa wafanyabiashara hao RUMANYIKA MANYANGA amesema wanashidwa kuendelea kimaisha na kiuchumi kutokana na na wengi wao kufanya biashara zenye vipato vidogo na wakati huo kutozwa fedha bila maelezo.
Aidha wameiomba serikali nakampuni zinazowasimamia polisi jamii kuwapatia fedha zionazokidhi mahitaji yao ili kupunguza usumbufu wanaowapatia wafanyabiashara hao.