WAFUGAJI WATAKIWA KUACHA KUVAMIA MAENEO YA HIFADHI

WAFUGAJI WATAKIWA KUACHA KUVAMIA MAENEO YA HIFADHI

Like
293
0
Wednesday, 05 November 2014
Local News

WAFUGAJI wa Jamii ya kimasai wametakiwa kufuata taratibu za kupata ardhi kihalali ,badala ya kuendelea kuvamia maeneo ya hifadhi yaliyopo kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu CHIKU GALAWA ambapo ameeleza uvamizi huo umekuwa kero pindi wanapotakiwa kuondoka kwenye maeneo hayo.

Amebainisha kuwa kwa kufuata taratibu itasaidia kuepusha migogoro isiyokuwa na tija ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo.

Comments are closed.