Wafungwa wateka gereza Sudan Kusini

Wafungwa wateka gereza Sudan Kusini

Like
680
0
Monday, 08 October 2018
Global News

Mamlaka nchini Sudan Kusini inaendelea na mazungumzo dhidi ya wafungwa ambao wamejihami kwa bunduki na visu, na ambao wanashikilia eneo la gereza hilo mjini Juba wakishinikiza kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais Salva Kiir.

Wafungwa hao walifanikiwa kuchukua Bunduki na visu kutoka ndani ya ghala la kuhifadhia silaha. Vikosi vya usalama vimelizingira gereza hilo ambalo pia ni makao makuu ya shughuli za wa taifa. Awali Rais Salva Kiir alitoa ahadi kwamba angeliwaachia wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa nchini humo jambo ambalo halijafanyika hadi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *