WAHITIMU 27005 WACHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA ARUSHA

WAHITIMU 27005 WACHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA ARUSHA

Like
256
0
Tuesday, 22 December 2015
Local News

JUMLA ya wanafunzi, 27005  ambao wamehitimu elimu ya msingi mwaka2015 mkoani Arusha wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2016.

 

Akitangaza matokeo hayo Kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha, Hamdouny Mansour, amesema jumla ya wanafunzi 33, 898 walifanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ambapo wavulana walikuwa ni 15, 868 na wasichana 18,030.

 

Mansour amesema waliofaulu wamepata  alama kati ya 100 hadi 250 ambapo wavulana ni12,563 na wasichana ni 14,442 na ufaulu huo ni sawa na asilimia 79.67 ikilinganishwa na mwaka 2014 ambapo kiwango cha ufaulu kilikuwa ni asilimia 67.69.

Comments are closed.