WAKULIMA MBEYA WAKABIDHIWA MASHINE ZA KUPANDIA MPUNGA KUKUZA KILIMO

WAKULIMA MBEYA WAKABIDHIWA MASHINE ZA KUPANDIA MPUNGA KUKUZA KILIMO

Like
810
0
Monday, 23 February 2015
Local News

WAKULIMA Wilayani Ileje Mkoani Mbeya wamepokea Mashine Sita za kupandia Mpunga zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 60 kwa ajili ya kuwezesha Kulima kwa kutumia Teknolojia bora ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Akikabidhi Mashine hizo kwa baadhi ya Vikundi vya wakulima katibu tawala FRANSIS MBEGILE amewataka wakulima hao kuzitumia vizuri na kuzitunza kwani watapata maelekezo ya namna ya kuzitumia

Kwa upande wake Kaimu afisa Kilimo mkoani humo HERMAN NJEJE amesema hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuendeleza kilimo wilaya sanjari na mpango wa kutekeleza kwa matokeo makubwa sasa katika sekta ya Kilimo.

Comments are closed.