WAMAMA KENYA WAANDAMANA KISA MMAMA MMOJA KUFUKUZWA KAZI KWA KOSA LA KUNYONYESHA MTOTO WAKE

WAMAMA KENYA WAANDAMANA KISA MMAMA MMOJA KUFUKUZWA KAZI KWA KOSA LA KUNYONYESHA MTOTO WAKE

Like
521
0
Tuesday, 15 May 2018
Global News

Nchini Kenya Wamama wameandamana leo mjini Nairobi kulalamika tuhuma za mwanamke mwenzao kufukuzwa eneo lake la kazi (Mgahawani) kwa sababu alinyonyesha mtoto wake akiwa kazini, jambo ambalo liliinua hasira kwa wakina mama wengi nchini humo na kufikia hatua ya kuanza kuingia barabarani wakielekea katika mgahawa huo, ambako mama huyo anatuhumu kuwa aliambiwa ajifunike wakati anamnyonyesha mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.
Mama huyo alieleza kwamba yeye alipokuwa ananyonyesha mtoto wake aliambiwa akanyonyeshee chooni, jambo lililomfanya ajione kama kadharauliwa.
Taarifa hiyo imezusha hisia kali kote nchini na kusababisha makundi ya kutetea haki za wanawake kuandaa maandamano ya leo mjini Nairobi.
Mgahawa huo umeomba utulivu udumishwe kufutia ghadhabu hiyo kubwa ya wanawake nchini ukiomba kupewa muda kulishughulikia suala hilo kwa ndani.
Mojawapo ya mashirika yalioshiriki maandamano hayo leo ni Muungano wa mawakili wanawake FIDA.
Unasema dhamira kuu ya maandamano ya leo ni kushinikiza haki za akina mama waungwe mkono na kusaidiwa katika kufanikisha kuwanyonyesha watoto wao bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Sheria ya afya nchini inaeleza kuwa waajiri wote nchini wanastahili kutenga nafasi kuwaruhusu wanawake kuwanyonyesha watoto wao katika maeneo ya kazi.
Kadhalika kampeni imeanzishwa kwenye mitandao ya kijamii kushinikiza haki za mama na mwana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *