WAMAREKANI WASHIKA MPINI WA BARAZA LA SENETI

WAMAREKANI WASHIKA MPINI WA BARAZA LA SENETI

Like
322
0
Tuesday, 04 November 2014
Global News

WAPIGA kura nchini Marekani wanashiriki katika uchaguzi, utakaoamua ni chama gani kitalidhibiti baraza la Seneti na kutoa sura ya muelekeo wa rais BARACK OBAMA katika kipindi cha miaka miwili iliosalia ya utawala wake.

Bwana OBAMA binafsi amesema anauangalia uchaguzi huo kuwa kipimo cha maoni ya wamarekani kuhusu sera zake.

Wagombea wa chama cha Republican wana matumaini kwamba kuvunjwa moyo kwa wapiga kura na sera za Bwana OBAMA kutawapa fursa ya kulidhibiti baraza la Seneti.

Kuna viti 36 kati ya100 vinavyogombewa katika uchaguzi huu na Warepublican wanahitaji viti sita kulidhibiti baraza hilo.

 

Comments are closed.