WANAFUNZI VYUO VIKUU KENYA WAAGIZWA KUTUMIA FACEBOOK NA TWITTER

WANAFUNZI VYUO VIKUU KENYA WAAGIZWA KUTUMIA FACEBOOK NA TWITTER

Like
310
0
Thursday, 06 November 2014
Global News

WASIMAMIZI wa Vyuo Vikuu nchini Kenya wameagizwa kufungua Mitandao ya Twitter na Facebook ambayo wanafunzi watatumia kutoa malalamiko yao kwa lengo la kuzuia machafuko katika Taasisi hizo.

Waziri wa Elimu nchini Kenya JACOB KAIMENYI amesema kuwa vifaa hivyo vya mawasiliano vitawasaidia wanafunzi kutoa malalamiko yao mbali na kupata majibu kutoka kwa Wasimamizi.

Waziri KAIMENYI ameshtumu mbinu zinazotumiwa na Vyuo Vikuu kukandamiza upinzani mbali na kudhibiti masuala ya wanafunzi kama vile Uchaguzi wao na kuwasingizia katika masuala ya utovu wa nidhamu bila kuwasikiliza.

Comments are closed.