WANAJESHI WA UINGEREZA WATUA SOMALIA

WANAJESHI WA UINGEREZA WATUA SOMALIA

Like
261
0
Monday, 02 May 2016
Global News

IMEELEZWA kuwa Wanajeshi wa Uingereza wamewasili nchini Somalia kusaidia katika juhudi za kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabaab.

Wanajeshi 10 waliowasili nchini Somalia ni sehemu ya kikosi cha umoja wa mataifa na watasaidia kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (Amisom) kukabiliana na Al-Shabaab.

Idadi ya wanajeshi wa Uingereza nchini Somalia inatarajiwa kupanda hadi 70 ambao watahusika na shughuli za matibabu, mipango na uhandisi.

Comments are closed.