WANAMGAMBO WA IS WASHAMBULIWA DIYABAKIR

WANAMGAMBO WA IS WASHAMBULIWA DIYABAKIR

Like
212
0
Monday, 26 October 2015
Global News

WANAMGAMBO wanne wanaotuhumiwa kuwa wa kundi la Dola la Kiislamu wameuwawa leo pamoja na polisi wawili wa Uturuki katika mashambuliano ya risasi yaliyotokea katika mji wa Diyabakir kusini mashariki mwa Uturuki.

Taarifa kutoka usalama zimesema kuwa polisi ilikuwa imefanya upekuzi kwenye nyumba kadhaa katika kitongoji cha mji huo ambapo inadhaniwa kwamba wapiganaji wa jihadi wamekuwa wakijificha na ndipo wanamgambo hao walipowafyatulia risasi polisi.

Hata hivyo mapigano makali bado yalikuwa yakiendelea na kwamba polisi ina hofu kuwa wanamgambo wengine huenda wakawa bado wamejificha katika eneo hilo.

Comments are closed.