WANANCHI WAMETAKIWA KUITUMIA SIKU YA UKIMWI KUPIMA AFYA ZAO

WANANCHI WAMETAKIWA KUITUMIA SIKU YA UKIMWI KUPIMA AFYA ZAO

Like
256
0
Wednesday, 25 November 2015
Local News

WITO  umetolewa kwa wananchi kote nchini kuyatumia maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba Mosi ya kila mwaka kupima afya zao ili kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho amesema  Siku ya Ukimwi Duniani nchini itaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi  kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya ugonjwa huo.

Comments are closed.