Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Rais JAKAYA KIKWETE wakati akifungua rasmi barabara ya Mwenge –Tegeta.
Naye Balozi wa Japani nchini MASAKI OKADA amezungumzia juu ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali yake na Tanzania
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 imegharimu kiasi cha Sh. bilioni 77.85, fedha
ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa
la JICA. Serikali ya Tanzania imechangia asilimia 7.64 katika gharama za ujenzi
wa Barabara hiyo.
Katika ufunguzi wa barabara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam SAIDI MECK SADIKI amesema kuwa hali hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa magari.
Naye Mhandisi Mkuu wa TANROAD PATRICK MFUGALE amesema ujenzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta imejengwa kwa kiwango chenye ubora