WANANCHI WAMETAKIWA KUVITUNZA NA KUVILINDA VYANZO VYA MAJI

WANANCHI WAMETAKIWA KUVITUNZA NA KUVILINDA VYANZO VYA MAJI

Like
234
0
Thursday, 12 February 2015
Local News

NAIBU Waziri wa Maji, Mheshimiwa AMOS MAKALLA amesema wananchi hawatafaidika na Miradi ya Maji inayotekelezwa na Serikali hivi sasa, kama hawatakuwa makini kuvitunza na kuvilinda vyanzo vya maji.

Mheshimiwa MAKALLA amezungumza hayo katika ziara yake Wilaya ya Babati, mkoa wa Manyara wakati akikagua Utekelezaji wa Miradi na kuzindua miradi iliyokamilika katika mkoa huo.

Amebainisha kuwa miradi hiyo inagharimu fedha nyingi na Serikali imedhamiria kuwapa wananchi Maji na siyo vinginevyo, lakini bila ushirikiano wao lengo halitafanikiwa.

MAKALA4 MAKALA2

Comments are closed.