KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani MOHAMED MPINGA ametoa onyo kwa baadhi ya Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii kuacha tabia ya kusambaza taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuthibitika kama zina ukweli ndani yake.
Kamanda MPINGA ameeleza hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu tukio la baadhi ya Mitandao kusambaza taarifa kuwa Basi la Dar Express limepata ajali hivyo kuleta taharuki kwa ndugu na abiria.