WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA

WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA

Like
291
0
Wednesday, 05 November 2014
Local News

RAIS  JAKAYA MRISHO KIKWETE amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa sanjari na kuhakikisha kuwa wanaisoma ipasavyo katiba inayopendekezwa ili kuelewa masuala muhimu yaliyopo kwenye katiba hiyo.

 

Rais KIKWETE ametoa wito huo mkoani Dodoma wakati akizungumza katika na Wazee mkoani humo ambapo amesema kuwa suala la wananchi kushiriki kikamilifu uchaguzi huo litasaidia katika kupata viongozi bora wenye kujali maslahi ya wananchi.

 

Mbali na hilo Rais Kikwete amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema katika kupambana na virusi hatari vya ugonjwa wa Ebola kwani hadi sasa hakuna dawa yoyote ya kuweza kutibu ugonjwa huo.

 

 

Comments are closed.