Wanasayansi wagundua mti mrefu zaidi duniani

Wanasayansi wagundua mti mrefu zaidi duniani

Like
802
0
Monday, 08 April 2019
Slider

Wanasayansi nchini Uingereza na Malaysia wanasema kuwa wamegundua mti mrefu zaidi duniani wenye urefu wa zaidi ya mita 100.

Mti huo wa kitropiki aina ya meranti ulipatikana katika msitu wa Borneo na kundi moja kutoka chuo kikuu cha Nottingham mwaka uliopita.

Watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Oxford walifanya utafiti huo kwa kutumia kamera zisizokuwa na rubani kuthibitisha rekodi hio.

Mti huo uliopatikana katika eneo la uhifadhi la Danum Valley huko Sabah umepewa jina Menara ambalo linamaanisha jumba refu.

Mkweaji miti kutoka eneo hilo, jami ambaye aliupima mti huo kwa kutumia kamba alisema alliogopa kuupanda mti huo

”Lakini kwa kweli picha kutoka juu ilikuwa nzuri mno. Sijui cha kusema isipokuwa tu ulikuwa uzoefu mzuri sana”, aliongezea.

Daktari Doreen Boyd, kutoka chuo kikuu cha Nottingham, alisema kuwa ugunduzi huo ulikuwa muhimu kwa kuwa ni sayansi inayosema miti kama hii inapatikana , ni mirefu hali ya kwamba hatukuwahi kudhania na huenda kuna miti mirefu zaidi ambayo haijagunduliwa.

”Inatuambia kwamba tunahitaji kuilinda miti”, alisema.

Daktari Alexander Shenkin , kutoka chuo kikuu cha Oxford , alisema baada ya kusikia ugunduzi huo walitembea kwa muda wa saa tatu hadi Menara.

Alisema: Nimeona kile ambacho wanasema ni miti mingi , lakini nilipotembea hadi katika mti huu, kichwa changu kilizidi kuangalia juu unapokaribia kileleni.

Sijawahi kuona mti mrefu kama huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *