WANASIASA WAMETAKIWA KUACHA KUPIGANA VIJEMBE NA MATUSI

WANASIASA WAMETAKIWA KUACHA KUPIGANA VIJEMBE NA MATUSI

Like
304
0
Wednesday, 30 September 2015
Local News

ZIKIWA zimebaki siku 24 kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani, baadhi ya Wananchi wamewataka wanasiasa kuacha kampeni za kupigana vijembe na matusi bali wafanye kampeni za kistaarabu.

Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema wanahitaji kusikia sera za vyama kupitia ilani za vyama hivyo na sio kufanya kampeni za kutupiana maneno na matusi jukwaani kwa kuwa wanasiasa wote lengo lao ni kujenga nyumba moja ambayo ni Tanzania ya awamu ya tano.

Comments are closed.