JESHI la Polisi Mkoani Arusha limewakamata watu kadhaa kwa kuhusishwa na tukio la Ujambazi wa kuteka mabasi sita ya abiria yaliyokuwa yanatoka nchini Kenya kuelekea Arusha nchini Tanzania.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, amesema katika Msako huo ulioanza juzi, wamefanikiwa kukamata watu hao katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Tukio la kutekwa kwa mabasi hayo lilitokea juzi usiku baada ya watu wanaodhaniwa kuwa majambazi kuvamia na kuteka mabasi hayo katika eneo la Mbuga Nyeupe, Wilaya ya Longido.