WASICHANA LONDON WAJIUNGA NA IS, UTURUKI YAISHUTUMU UINGEREZA

WASICHANA LONDON WAJIUNGA NA IS, UTURUKI YAISHUTUMU UINGEREZA

Like
248
0
Tuesday, 24 February 2015
Global News

UTURUKI imeshutumu Uingereza kwamba imechukua muda mrefu kuijulisha nchi hiyo kuhusu wanafunzi wa kike watatu waliokuwa wakisoma London Uingereza kwamba walisafiri kwenda nchini Syria kwa lengo la kujiunga na Islamic State.

Inaelezwa kuwa wanafunzi hao walipanda ndege ya shirika la ndege la Uturuki kutoka Uingereza na walihitaji hati ya kusafiri na visa kuingia Uturuki.

Sakata la wanafunzi hao wa kike kutoka London kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State limekuwa likishtua wengi. Huku serikali ya Uturuki inasema ingechukua hatua kama ingepewa taarifa mapema .

Comments are closed.