WATANO MBARONI KWA UCHOCHEZI WA VURUGU SAKATA LA JKT

WATANO MBARONI KWA UCHOCHEZI WA VURUGU SAKATA LA JKT

Like
293
0
Monday, 23 February 2015
Local News

JESHI la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewakamata vijana wapatao wa tano wanao jiita viongozi wa umoja wa kikundi cha wahitimu wa mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa JKT kwa makosa ya uchochezi na mikusanyiko isiyo ya halali.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es salaam na Kamishna wa polisi kanda hiyo suleman kova ambapo amesema kuwa lengo la kikundi cha wahitimu hao kufanya mikusanyiko hiyo nikutaka kuandamana kwenda Ikulu kuonana na Rais Dkta JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa madai ya kupatiwa majibu yao ya tatizo la ajira ya kudumu.

Aidha Kamishina kova amefafanua kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa umoja huo hauna usajiri kisheria na hakuna ahadi yeyote ambayo kikundi hicho kimepewa mpaka sasa.

Comments are closed.