WATANZANIA WATAKIWA KUWATUMIA WATAALAMU WA UBUNIFU MAJENGO NA UKADIRIAJI

WATANZANIA WATAKIWA KUWATUMIA WATAALAMU WA UBUNIFU MAJENGO NA UKADIRIAJI

Like
376
0
Monday, 15 December 2014
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuwatumia wataalamu wa ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi katika ujenzi ili kuepusha uwepo wa majengo yalio chini ya kiwango yanayoweza kuhatarisha maisha ya watu na mali zao.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Msajili wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi JEHAD JEHAD alipozungumza katika mkutano wa wadau wa taaluma na bodi hiyo ambapo amesema Watanzania wengi wamekuwa wakijenga kiholela kwa kuhofia gharama bila kujali kuwa ujenzi huo unagharama zaidi endapo jengo litadondoka.

Aidha JEHAD amesema kuwa bodi hiyo inashughulikia zaidi majengo yenye gharama ya zaidi ya milioni 150 pamoja na majengo ya huduma za kijamii ikiwemo Shule, Hospitali na Masoko lakini pia amewashauri watanzania kuwatumia wataalamu hao kwa majengo binafsi.

 

Comments are closed.