Watoto wafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo wakiwa tumboni mwa mama zao Uingereza

Watoto wafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo wakiwa tumboni mwa mama zao Uingereza

Like
964
0
Wednesday, 24 October 2018
Global News

Watoto wawili ambao bado hawajazaliwa wamefanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo wiki chake kabla ya kuzaliwa kwao.

Upasuaji huo ambao ni wa kwanza wa aina hiyo nchini Uingereza ulifanywa na kundi la madaktari 30 kati chuo kimoja jijini London.

Watoto hao walikuwa na tatizo lilalojulikana kama spinal bifida, ambapo uti wa mgongo hukosa kukua vile inavyotakikana.

Mara nyingi hali hiyo hutibiwa baada ya mtoto kuzaliwa lakini ikiwa itatibiwa mapema hali ya afya ya mtoto huwa bora zaidi.

Wakati wa upasuaji huo uliochukua muda wa dakika 90, madaktari walipasua tumbo la mama kisha wakashona pamoja sehemu ya uti wa mgongo wa mtoto iliyokuwa imeachana.

Upasuaji huo ni hatari sana na unaweza kusababisha mama apatwe na machungu ya mapema ya kujifungua.

Mama wajawazito amabo watoto zao waligundulika na shida hiyo nchini Uingereza walihitaji kwenda ng’ambo Marekani, Ubelgiji au Uswizi kufanyiwa uposuaji huo hapo kabla.

“Ni kitu kizuri. Wanawake sasa hawahitaji kusafiri kwenda Uingereza. Wanaweza kuwa na familia yao, na gharama ni ya chini. Kwa hivyo mambo yote ni mazuri,”alisema Prof David

Spina bifida ni nini?

Kulingana na shirika la Charity Shine, zaidi ya watoto 200 huzaliwa na hali hiyo ya spina bifida kila mwaka.

Hali hiyo hutokea wakati kitu kinachoitwa neural tube – awamu ya kwanza ya kukua kwa ubongo na uti wa mgongo hukua kwa njia isiyostahili na husababisha kuwepo nafasi kwenye uti wa mgongo.

Upasuaji unaweza kutumia kuziba nafasi hiyo kwenye uti wa mgongo mara nyingi, lakini mara nyingi matatizo yatakuwa tayari yametokea na miguu kupooza.

Baadhi ya watu hupatwa na hali ngumu ya kujifunza.

Kinachosababisha hali hiyo hakijulikani, ambayo hutokea wakati wa mimba.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *