WATOTO WANAOTUMIWA NA WALEMAVU KUOMBA MISAADA HUSHINDWA KUHUDHURIA MASOMO

WATOTO WANAOTUMIWA NA WALEMAVU KUOMBA MISAADA HUSHINDWA KUHUDHURIA MASOMO

Like
285
0
Friday, 01 April 2016
Local News

IMEBAINIKA kuwa asilimia kubwa ya watoto wanaotumiwa na watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuomba fedha barabarani wanashindwa kuhudhuria masomo kutokana na kutumia muda mwingi kwa kazi hiyo.

Akizungumza na EFM   mwanaharakati wa masuala ya watu wenye ulemavu, Jonathan Haule amesema kuwa watoto hao wamekuwa wakitembea barabarani nyakati za masomo.

Amesema kuwa ni vyema serikali ikaanzisha mifumo madhubuti itakayowawezesha watu wenye ulemavu kufanya kazi zao pasipo kutegemea msaidizi.

Comments are closed.