WAZANZIBARI WAHIMIZWA KUIPIGIA KURA YA NDIO KATIBA MPYA

WAZANZIBARI WAHIMIZWA KUIPIGIA KURA YA NDIO KATIBA MPYA

Like
231
0
Tuesday, 20 January 2015
Local News

KATIBU MKUU wa Chama cha Mapinduzi –CCM, Abdulrahman Kinana, amewahimiza Wazanzibari kuipigia kura ya ndiyo Katiba mpya iliyopendekezwa kwakuwa inatatua kero nyingi za wanzanzibari  katika muungano na kuwafanya wawe na uhuru zaidi.

Bwana kinana amefafanua umuhimu wa kuipigia kura katiba hiyo pendekezwa huku akitolea mifano ya  Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iwapo Rais wa Jamhuri atatoka Bara, Zazibar kujiunga na jumuiya za kimataifa bila kikwazo, kuwa na uhuru wa kukopa na mambo mengine mengi yaliyomo katika katiba hiyo.

Kinana  alikuwa katika Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2010, Katika mikutano mbalimbali ambayo amekuwa akihutubia na kuzungumza na wananchi na wana CCM amekuwa akihimiza viongozi kufuata maadili ya uongozi jambo ambalo ni muhimu na la lazima katika uongozi ili kuutumikia umma katika misingi mizuri na yenye tija.

 

Comments are closed.