WAZIRI KAIRUKI AAGIZA WATUMISHI KUJENGEWA UWEZO

WAZIRI KAIRUKI AAGIZA WATUMISHI KUJENGEWA UWEZO

Like
250
0
Tuesday, 22 December 2015
Local News

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora mheshimiwa Angella Kairuki ameagiza kuzingatiwa kwa utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi ili waweze kumudu majukumu katika sehemu zao za kazi.

 

Waziri Kairuki ameyasema hayo wakati wa kikao kazi na Idara ya uendelezaji Rasilimali watu na kusisitiza kuwa waajiri wasitegemee serikali kuruhusu kuendelea kutoa mikataba kwa watumishi wakati mpango wa urithishanaji madaraka upo na watumishi wenye sifa stahiki wapo.

 

Mbali na hayo ameelekeza uchunguzi ufanyike kubaini watumishi wanaotarajiwa katika nafasi za uongozi ili kujiridhisha kwa sifa walizonazo na endapo kuna upungufu waandaliwe mapema kwa taratibu zilizopo kwa manufaa ya wote.

Comments are closed.