WAZIRI MBARAWA AZITAKA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA YAKE KUFANYA KAZI KWA WELEDI

WAZIRI MBARAWA AZITAKA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA YAKE KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Like
234
0
Friday, 26 February 2016
Local News

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezitaka taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa uwazi, weledi na uaminifu ili kuongeza mapato na kutimiza adhma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

 

Prof. Mbarawa ametoa wito huo mkoani Kilimanjaro katika majumuhisho ya ziara yake ya mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro iliyolenga kukagua miradi ya ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, Posta, TTCL, TBA na TEMESA.

 

Waziri Mbarawa amewataka mameneja na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupima utendaji kazi wa kila mfanyakazi na kusisitiza zile taasisi zinazozalisha upimwaji utazingatia ukusanyaji wa mapato.

Comments are closed.