WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA KIKAZI RUVUMA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA KIKAZI RUVUMA

Like
331
0
Monday, 04 January 2016
Local News

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameanza ziara yake ya kikazi leo Mkoani Ruvuma.

 

Waziri Mkuu Majaliwa aliondoka na kuwasili Mkoani humo jana, na leo atafungua tawi la Benki ya Posta Mjini Songea pamoja na kukagua Maghala ya wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula-NFRA, Kanda ya Songea.

 

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kesho anatarajiwa kutembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo na kuongea na watumishi wa Hospitali hiyo kabla ya kuanza safari yake ya kurejea jijini Dar es salaam siku ya Jumatano.

 

Comments are closed.