WAZIRI Mkuu wa Australia Tony Abbot amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.
Waziri Mkuu Abbot ametoa pongezi hizo mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais Kikwete namna nchi hizo mbili zinavyoweza kuendelea kushirikiana katika kulinda usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii.
Rais Kikwete yuko nchini Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove ambapo leo baada ya chakula cha mchana atapanda mti kuashiria kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili kwa kipindi kirefu kijacho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kijeshi wa Fairbairn mjini Canberra katika siku ya mwanzo ya ziara yake Rasmi ya siku nne ya Kiserikali nchini Australia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua na kutoa heshima katika kaburi la askari wa Australia wakati alipotembelea jumba la Makumbusho ya Taifa ya vita – Australian War Memorial