WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA KUTEMBELEA KIWANDA CHA TAMCO LEO

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA KUTEMBELEA KIWANDA CHA TAMCO LEO

Like
402
0
Thursday, 02 July 2015
Local News

WAZIRI MKUU wa Ethiopia Heilemariam Disalegn Boshe leo anatembelea Kiwanda cha kutengeneza Dawa za Kuulia Wadudu-TAMCO- kilichopo Kibaha Mkoani Pwani akiongozana na Mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Ziara hiyo ya siku mbili ni sehemu ya Mapambano ya Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Nchi ya Ethiopia dhidi ya Mazalia ya Mbu ili kudhibiti kuenea kwa Ugonjwa wa Malaria ambapo Waziri Mkuu Boshe ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria.

Mheshimiwa Boshe amewasili jana usiku.

Comments are closed.