WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ISRAEL AHUKUMIWA MIEZI 18 JELA

WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ISRAEL AHUKUMIWA MIEZI 18 JELA

Like
205
0
Tuesday, 29 December 2015
Global News

WAZIRI MKUU wa zamani wa Israel Ehud Olmert ametakiwa kutumikia kifungo cha miezi 18 jela kwa makosa ya rushwa.

Olmert alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela na mahakama mwaka 2014, lakini adhabu hiyo sasa imepunguzwa na Mahakama ya Juu.

Mwanasiasa huyo wa umri wa miaka 70 alipatikana na hatia kuhusu mkataba wa ujenzi wa nyumba ambao ulifanyika alipokuwa meya wa Jerusalem, kabla yake kuwa waziri mkuu 2006.

Comments are closed.