Msanii kutoka Nigeria ambae amekuwa nnchini kwa kipindi kisichopungua wiki moja ambapo alikwenda kufnya show pamoja na kushiriki kwenye uaandaaji wa video mpya ya Victoria kimani katika wimbo alioshirikishwa.
Taarifa kutoka kwenye chapisho la Standard Digital huko kenya limeeleza kuwa wiz kid alikamatwa katika hoteli ya Nairobi Crown Plaza mwishoni mwa wiki ambapo ndio hoteli aliyofikia.
mtandao huo umeeleza ya kuwa mambo yalikwenda mbali zaidi baada ya wafanya kazi hao kutaka kumpeleka polisi msanii huyo kitendo ambacho kilipelekea polisi waitwe kumkamata na kumweka chini ya ulinzi kwa masaa kadhaa na kumuhoji katika kituo cha Capital Hill Police.
wakati hayo yakiendelea jina la Victoria Kimani limekuwa likitajwa pia kufuatia pia mara baada ya kwenda polisi pia muda mfupi baada ya wiz kid kukamatwa.
Wiz kid alitozwa elfu hamsini za Kenya kama sehemu ya faini baada ya kukutwa na hatia ya kuvuta bangi katika hoteli hiyo na baadae kurejea Lagos
hadi sasa hakuna alietaka kuzungumzia tukio hilo kati ya Victoria na Wiz kid mwenyewe