WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI YAANDAA WARSHA KUENDELEZA STADI ZA KAZI

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI YAANDAA WARSHA KUENDELEZA STADI ZA KAZI

Like
341
0
Thursday, 26 November 2015
Local News

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi na Ajira imeandaa warsha ilinayolenga kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa miaka 10 wa kuendeleza stadi za kazi kwa miaka mitano ya kwanza.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam leo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Elimu ya juu kutoka Wizara hiyo Dokta Jonathan Mbwambo amesema kuwa takwimu zinaonesha Tanzania ina watu wenye ujuzi wa chini na stadi za kazi ambazo zinahitaji kukuzwa ili nchi iweze kufikia matarajio yake.

Aidha Mbwambo ameongeza kuwa changamoto za stadi za kazi zinasababisha zaidi ya Vijana milioni 14kushindwa kuwa na shughuli za kipato cha kuridhisha na hivyo kuibua malalamiko dhidi ya mfumo wa elimu.

Comments are closed.