WIZARA YA FEDHA YATILIANA SAINI MIKATABA NA BENKI YA DUNIA

WIZARA YA FEDHA YATILIANA SAINI MIKATABA NA BENKI YA DUNIA

Like
255
0
Thursday, 12 March 2015
Local News

WIZARA ya fedha imetiliana saini mikataba mitatu na benki ya dunia itakayowezesha kuipatia serikali ya Tanzania mikopo ya miradi mitatu ya kuendeleza jiji la Dar es salaam, mradi wa kuendeleza ujenzi wa nyumba za bei nafuu na mradi wa uvuvi wa kikanda wa kuendeleza uvuvi, yenye ujumla ya thamani ya dola milioni 396 sawa na shilingi bilioni 710.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Katibu mkuu wa wizara ya fedha Dokta Servacius Likwelile ameahidi kuwa serikali itasimamia kuhakikisha kuwa utekelezaji unaanza maramoja ili kuleta manufaa kama ilvyokusudiwa.

Comments are closed.