HATIMAYE leo wananchi wa Zambia wanapiga kura kuchagua Rais wa nchi hiyo, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Michael Sata Oktoba mwaka jana.
Chama tawala cha PF kinauhakika wa kushinda katika uchaguzi huo licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka upinzani.
Waangalizi wa kikanda katika uchaguzi huo, wanasema wameridhishwa na maandalizi ya zoezi zima la upigaji kura.Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kati ya Edgar Lungu anayegombea nafasi hiyo kupitia chama tawala na mpinzani wake HAKAINDE Hichilema kutoka United Party for National Development.