ZIMBABWE: WALIOMUUA SIMBA CECIL KUSHTAKIWA

ZIMBABWE: WALIOMUUA SIMBA CECIL KUSHTAKIWA

Like
265
0
Wednesday, 29 July 2015
Global News

WATU  wawili wanaume wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baadaye leo wakishtakiwa kwa makosa ya uwindaji , baada ya simba maarufu nchini humo kuuawa na mtalii mmoja raia wa Marekani .

Simba huyo, anayejulikana kwa jina la Cecil, alipigwa risasi nje kidogo ya mbuga ya wanyama ya taifa ya Hwange na Walter Palmer, daktari wa meno na mtu anayependa uwindaji, ambaye pia anaweza kukabiliwa na mashtaka.

Maandamano juu ya kuuawa kwa simba huyo yamefanyika nje ya makaazi ya bwana Palmer katika jimbo la Minnesota nchini Marekani, lakini yeye amesema anajuta kwa kumpiga risasi , lakini akasema alidhani alikua katika mawindo halali.

 

Comments are closed.