ZUMA KUKUTANA NA WADAU WA ELIMU

ZUMA KUKUTANA NA WADAU WA ELIMU

Like
214
0
Friday, 23 October 2015
Global News

RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepangiwa kukutana na viongozi wa wanafunzi wa vyuo leo kujadili maandamano ya wanafunzi yaliyosababishwa na kuongezwa kwa ada ya masomo.

Wanafunzi wamekuwa wakiandamana wiki moja sasa, hasira nyingi zikielekezwa kwa chama tawala African National Congress (ANC).

Jana, maelfu ya wanafunzi walikusanyika nje ya makao makuu ya ANC mjini Johannesburg wakitaka elimu itolewe kwa wote bila malipo yoyote.

Comments are closed.