Watu zaidi ya 130 wamefariki nchini Canada kutokana na joto lisilo la kawaida kupiga ambalo limevunja rekodi ya kiwango cha joto. Polisi wa British Columbia wamepokea taarifa za vifo tangu Jumatatu, vifo vingi vikijumuisha wazee. Wanasema kiwango hicho cha joto kupiga katika eneo hilo kilisababisha vifo hivyo. Jumanne, kiwango cha joto nchini Canada kiliongezeka zaidi ikawa siku ya tatu mfululizo -ilikuwa nyuzi joto 49.5 huko Lytton, British Columbia. Kabla ya wiki hii , kiwango cha joto cha Canada hakikuwahi kuvuka...
Matamshi ya mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles ‘Jaguar’ Kanyi kuhusu kuwatishia raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Kenya yaliwasilishwa mbele ya kikao cha bunge ili kujadiliwa. Hatua hiyo inajiri huku Mbunge huyo akizuiliwa katika kituo cha polisi usiku kucha ambapo anasubiri kuwasilishwa mahakamani siku ya Alhamisi. Kulingana na mtandao wa runinga ya Citizen nchini Kenya, licha ya wabunge wengi kushutumu jinsi ambavyo bwana Jaguar alitoa hoja yake , baadhi yao walikubaliana kwamba kuna swala tata kuhusiana na raia wa...
Ukungu (fangasi) – ambao umeboreshwa kisayansi kutoa sumu ya buibui – unaweza kuua idadi kubwa ya mbu wanaoambukiza malaraia, utafiti mpya wa kisayansi umebaini. Majaribio ya ukungu huo, ambayo yamefanyika nchini Burkina Faso, Afrika Magharibi yameonesha kuwa idadi ya mbu iliteketezwa kwa 99% ndani ya siku 45. Watafiti wanasema si lengo lao kutokomeza mbu hao bali kusaidia kuzuia maambukizi ya malaria. Ugonjwa wa malaria, unaoambukizwa na mbu jike aina ya Anopheles wanyonyao damu huua zaidi ya watu 400,000 kwa mwaka....
Mwanaume mmoja raia wa Japan, amepoteza maisha ndani ya Ndege akitokea Mexico City baada ya kumeza kete 246 za Cocaine. Ndege hiyo, iliyokuwa ikielekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Narita nchini Japan ililazimika kutua kwa dharura katika jimbo la Sonora nchini Mexico mwanaume huyo alipoanza kupoteza fahamu. Mamlaka zimesema mtu huyo aliyejulikana kwa jini la Udo N, alipoteza maisha baada ya ubongo wake kujaa maji kutokana na matumizi ya madawa kupita kiasi. Kwa mujibu wa taarifa ya mwanasheria...
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, David Kafulila ameutaka mpango kazi wa kuratibu taasisi na mashirika yanayotoa msaada wa kisheria kwa wananchi ukamailike haraka ili wananchi wapate huduma ya usaidizi wa kisheria kwa ufanisi. Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa msaada wa kisheria kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Songwe. “Watu wengi wamepoteza haki zao kwa kutokujua sheria au kutokuwa na fedha za kumudu gharama za mawakili lakini serikali imetengeneza...
Mchezaji soka Saido Berahino amepatikana na hatia ya kuendesha gari huku akiwa amekunywa pombe. Mshambuliaji wa Stoke City alikuwa amezidisha takriban mara tatu ya kiwango cha kileo wakati wakati gari lake aina ya Range Rover liliposimamishwa katika eneo la West End jijini London majira ya saa tisa usiku tarehe 18 Februari. Mahakama ya Highbury Corner ilisikiliza kesi ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 25-ambaye alikamatwa dakika chache baada ya kuibiwa. Mahakimu walisema”hakuwa na uoga wa kifo wala wa kujeruhiwa...
Bunge la Afrika Mashariki (EALA) limepitisha azimio linalotoa wito wa kuwekwa kwa marufuku dhidi ya watengenezaji na waagizaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone. Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni, mafuta na urembo wenye kemikali ya hydroquinone inayobadilisha ngozi kuwa nyeupe. Hydroquinone ni kemikali inayopatikana katika aina mbali mbali za bidhaa mbali mbali za mwili ambayo kwa kawaida imetengenezwa kwa ajili ya kuifanya ngozi kuwa nyeupe. “Athari za vipodozi vyenye hydroquinone zinaonekanana zimesambaa katika jumuiya nzima ya...
Wanasayansi nchini Uingereza na Malaysia wanasema kuwa wamegundua mti mrefu zaidi duniani wenye urefu wa zaidi ya mita 100. Mti huo wa kitropiki aina ya meranti ulipatikana katika msitu wa Borneo na kundi moja kutoka chuo kikuu cha Nottingham mwaka uliopita. Watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Oxford walifanya utafiti huo kwa kutumia kamera zisizokuwa na rubani kuthibitisha rekodi hio. Mti huo uliopatikana katika eneo la uhifadhi la Danum Valley huko Sabah umepewa jina Menara ambalo linamaanisha jumba refu. Mkweaji...
Maandamano yamekumba mji wa mpakani wa Namanga uliopo kati ya kenya na Tanzania. Kulingana na maafisa wa polisi maandamano hayo yalizuka kufuatia kutekwa nyara kwa mfanyibishara mmoja wa Kenya ambaye waandamanji hao wanasema alipelkekwa nchini Tanzania. Mfanyikazi wa ofisi ya serikali katika mji huo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa waandamanaji hao waliojawa na ghadhabu walifunga barabara inayoelekea Tanzania na hivyobasi kukatiza uchukuzi kutoka na kuelekea nchini humo. Anasema hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi wakati maafisa...
Serikali wilaya ya Mtwara Mjini imewatahadharisha wafanyabiashara wilayani humo kwa kuwataka kila mmoja kutambua wajibu wake, ambapo hatua kali zitakuchuliwa kwa atakayekutwa hana Leseni wala Kitambulisho cha msamahama wa Kodi kama ilivyoelekezwa na Rais Dkt. Magufuli Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda katika kikao na Watendaji wa Kata na Mitaa wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, kikao kilicholenga kuwahamasisha watendaji hao kutoa elimu kwa wananchi kuwataka kuchangamkia Vitambulisho vya wajasiliamali vilivyotolewa na Rais....
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano ni Serikali inayojali wananchi wake hivyo kuanzia sasa amesitisha zoezi zima la kubomoa makazi ya watu yaliyojengwa bila kufuata mpango mji. Rais ameelekeza kuwa nyumba hizo zisibomolewe kwa kuwa hayakuwa makosa yao kujenga katika maeneo hayo na kuelekeza kuwa watu wote wasio na hati miliki za ardhi kufanyiwa urasimishaji wa makazi yao. ”Serikali ya awamu ya tano kuanzia sasa haitabomoa tena nyumba...