AMAVUBI KUINGIA MWANZA JAN 21TAYARI KUKIPIGA NA STARS

AMAVUBI KUINGIA MWANZA JAN 21TAYARI KUKIPIGA NA STARS

Like
252
0
Saturday, 17 January 2015
Slider

Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) inatarajiwa kuwasili katika jiji la Mwanza, Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars ambapo nyasi zitawaka moto kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura, Amavubi yenye msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itawasili kwa ndege ya RwandAir na siku hiyo hiyo jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya JB Belmont.

Baada ya kocha Mdachi, Mart Nooij kutaja kikosi, Stars inaingia kambini keshokutwa (Januari 18 mwaka huu), na siku inayofuata itakwenda Mwanza tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayofanyika Januari 22 mwaka huu.

Kikosi hicho cha Kocha Mart Nooij ambacho ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo za michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) kinaundwa na wachezaji 26.

Comments are closed.