Katika kuadhimisha Siku ya makazi Duniani Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewataka Wananchi kufuata sheria na taratibu za ujenzi maeneo ya Mijini ili kuepuka na hasara pamoja na usumbufu wa kubomolewa makazi yao.
Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Waziri wa Wizara hiyo Profesa ANNA TIBAIJUKA
Amebainisha kuwa kupitia mradi wa kuboresha Miundombinu kwa kushirikiana na jamii kuna baadhi ya maeneo yameboreshwa
Kauli mbiu isemayo, SAUTI KUTOKA MAKAZI DUNI.