Polisi wakatazwa kuwashambulia waandamanaji Sudan

Polisi wakatazwa kuwashambulia waandamanaji Sudan

Like
606
0
Wednesday, 10 April 2019
Global News

Polisi nchini sudan imewaamuru maafisa wake kutowashambulia maelfu ya waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu wa jeshi mjini Khartoum tangu Ijumaa.

Waandamanaji hao wanamtaka rais Omar al-Bashir ajiuzulu.

Awali milio ya risasi ilisikika nje ya makao ya jeshi na ripoti zinasema kuwa maaskari wanaotoa ulinzi kwa waandamanaji wamepigwa risasi na maajenti wa serikali.

 

Katika taarifa yake msemaji wa polisi aliandika”Tunatoa amri kwa vikosi vyote” visiingilie “maandamano ya amani aukuwashambulia wananchi”.

“Tunamuomba Mungu asaidie kuleta utulivu nchini mwetu… na kuwaunganisha Wasudan… na kufikiwa kwa makubaliano yatakayosaidia kupokezana madaraka kwa amani,” iliendelea kusema taarifa hiyo.

Waziri wa mambo ua ndani wa nchi hiyo amesema waandamanaji saba waliuawa siku ya Jumatatu na wengine 15 kujeruhiwa, huku maafisa 42 wa vikosi vya usalama nao wakijeruhiwa pia.

Ameongeza kuwa karibu watu 2,500 wamekamtwa.

Mmoja wa wandamanani hao, Ahmed Mahmoud, ameimbia BBC kuwa maajenti wa kitaifa wa upelelezi walitumia mabomu ya kutoza machozi na risasi halisi dhidi ya waandamanaji.

Amesema maaskari wamewatengea eneo salama waandamanaji karibu na makao makuu ya jeshi la taifa.

“Hakuna haja ya Omar al-Bashir kutumumia majangili wake kutuondoa barabarani, hatuendi popote,” alisema.

Mwandamanaji mwingine ameiambia BBC kuwa sio kila mwanajeshi ana unga mkono vugu vugu la maandamano; Maafisa wa ngazi ya juu jeshini wanaunga mkono serikali iliyopo madarakani, huku wale wa ngazi ya chini wakiunga mkono waandamanaji.

Siku ya Jumatatu kuliibuka video inayowaonesha maafisa wakifyatua risasi kuelekea sehemu ambayo haikubainika huku waandamanaji wakijificha nyuma yao.

 

Waandamanaji walisema kuwa maafisa hao walikuwa wanajibu mashambulio kutoka kwa maajenti wa NISS.

Kumekuwa na miito ya kuitaka serikali ya Sudan kutotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia.

Marekani, Uingereza na Norway yametoa wito kwa serikali kutoa suluhisho la mpito la kisiasa.

”Ni vyema serikali ishughulikie matakwa ya wandamanaji kwa njia “ya uwazi na uwajibikaji”, ilisema taarifa yao.

“Kutofanya hivyo kutasababisha machafuko. Mamlaka nchini Sudan ina jukumu la kuzua matukio kama hayo,” iliendelea kusema taarifa yao..

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa pande zote mbili “kuwa na subira ili kuzuia kuzuka kwa machafuka”.

Mwandishi habari Mohamed Ali Fazari, aliyekuwepo katika umati wa waandamanaji mjini Khartoum, anasema waanadamanaji hao wanaliomba jeshi lishirikiane na raia dhidi ya serikali.

Umati ulipiga kelele ukisema “uhuru, uhuru, haki – jeshi moja, watu wamoja”, ameiambia BBC.

Kiini cha maandamano hayo awali kilitokana na gharama kubwa ya maisha lakini sasa ni ya kumshinikiza rais Bashir ambaye amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30 sasa, ajiuzulu.

Uchumi wa Sudan umeathirika kwa muda mrefu na vikwazo vya Marekani kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita inayoishutumu Khartoum kwa kufadhili makundi ya kigaidi.

Utawala wake umegubikwa kwa shutuma za uikukaji wa haki za binaadamu.

Mnamo 2009 na 2010, mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) ilimshtaki kwa makosa ya uhalifu wa kivita, mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binaadamu.

Marekani iliiwekea vikwazo Sudan kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita kwa tuhuma za kufadhili makundi ya kigaidi.

Mnamo Desemba mwaka jana serikali ya Sudan ilitangaza kwamba bei ya mafuta na mkate itapanda.

Katika mwaka uliofuata uamuzi huu, gharama ya maisha ilipanda huku pauni ya Sudan ikashuka thamani kwa kiasi kikubwa.

Tangazo la kupanda kwa bei ya bidhaa hizo ilichangia kuzuka maandamano, yaliogeuka kuwa shinikizo dhidi ya Bashir ajiuzulu.

Mwezi Februari kulikuwana fununu rais Omar al Bashiri atajiuzulu lakini katika hotuba yake kwa taifa rais huyo alitangaza hali ya hatari kote nchini humo

Maandamano ya hivi punde yanajiri huku taifa hilo likiadhimisha ukumbusho wa 34 wa mapinduzi yaliyoondoa madarakani utawala wa rais wa zamani wa Sudan Jaafar Nimeiri.

cc;-BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *