BUNGE LARIDHIA ITIFAKI YA KUANZISHA TUME YA UTAFITI WA AFYA AFRIKA MASHARIKI

BUNGE LARIDHIA ITIFAKI YA KUANZISHA TUME YA UTAFITI WA AFYA AFRIKA MASHARIKI

Like
345
0
Friday, 14 November 2014
Local News

 

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Azimio kuhusu Tanzania kuridhia itifaki ya kuanzisha tume ya utafiti wa Afya katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuiwezesha Jumuiya kupata ushauri wa masuala ya kiafya hali itakayoimarisha huduma hiyo kwa wananchi.

Akitoa Hoja rasmi ya Azimio hilo leo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta SEIF RASHID amesema umuhimu wa azimio katika utekelezaji wa Utafiti huo utakuwa katika kiwango cha kuridhisha katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za Kiafya.

Katika uchangiaji wa hoja hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani kupitia kwa Mbunge wa jimbo la Sunve, Mwanza, Richard Ndasa imeonesha hofu ya kufanikiwa kwa utafiti huo kutokana na rekodi za tafiti mbalimbali zilizopita.

 

Comments are closed.